Kilimo shadidi (System of rice intensification {SRI}), Mbinu ya Kisasa Kilimo cha Mpunga

SRI hybrid rice field


    Fuatana nami katika kujifunza jinsi unavyoweza badili kutoka kulima mpunga kimazoe kwenda katika kilimo chenye kutoka mavuno tele kwa
mbinu za karne ya 21. Kilimo shadidi (System of rice intensification).

HISORIA YA KILIMO SHADIDI (SRI) CHA MPUNGA

System of rice intensification (SRI) au kilimo shadidi kwa kiswahili ilivumbuliwa kwa mara ya kwanza Madagasca na kasisi Fr. Henri de Laulanié mwaka 1960. Kanuni hii imeounyesha uwezo mkubwa sana kila mahala duniani ilipotumika.


KILIMO SHADIDI ( SRI) ILIPOVUNJA REKODI YA DUNIA KWA MARA YA KWANZA.

Rekodi ya uzalishaji wa mpunga duniani haishikwi na Vyuo vya utafiti wa kilimo, wala wakulima wakubwa marekani. Ni mkuma mmoja kutoka katika kijiji cha Darveshpura nchini india. Kwa kutumia kanuni hii alivunja rekodi ya dunia kwa kuzalisha tan 22.4 (magunia 224) kwa hekari moja rcordi iliyokuwa ikishikiliwa na mchina ni 19 tani (magunia 190 kwa heka). Wastani wa mavuno kwa dunia kwa kutumia SRI duniani ni tani 4 (magunia 40 kwa heka).


SIRI NA FAIDA ILIYOJIFICHA NYUMA YA KILIMO SHADIDI
  1. Punguza msongamano wa miche, Panda mche mmoja mmoja kwa nafasi ili mizizi na shina vipate nafasi ya kutosha kukua.
  2. Utumizi wa maji kidogo kwa kilimo cha umwagiliaji hivyo unaeza kutumia maji kwa shughuli nyingine
  3. Unaweza kupanda eneo kubwa kwa kutumia mbegu chache
  4.  Mazao yatatoka mengi na ni vigumu kupata magonjwa (mara mbili zaidi ya njia ya kawaida)
  5.  Njia hii inaboresha ardhi na palizi lake linaifanya ardhi iwe na rutubaz zaidi.

MAANDALIZI YA KITALU 


panda mbegu zako vizuri katika kitalu kwa njia ya kawaida. Mbegu za kupanda kwa mfumo huu zinashauliwa kupandwa zikiwa bado ndogo zenye umri wa siku zisizozidi 8 hadi12. Pengine kwa kutaka kuharakisha zaidi, loweka mbegu zikiwa ndani ya mfuko wa sandarusi kwa saa 24, zitoe kisha ziache kwa siku moja na unyevu hadi zitakapoanza kutoa mizizi kisha upeleke wa kitalu.

 UPANDWAJI WA MICHE SHAMBANI



Mche mmoja mmoja unapandwa kwa ubali wa 24 cm, au mraba mdogo wenye urefu na upana wa cm 24 au 30 katika kila kona ya mraba kama inavyoonekana hapa chini.




    UPALILIAJI

Palizi ni Muhimu kuhakikisha unapata mazao mengi. Katika SRI palizi hufanywa kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho Paddy Weeder Machine. Vibarua watatu kwa kutumia kifaa hiki wanaweza kumaliza herkari moja kwa muda mfupi. Njia nyingine pia zaweza kutumika.



paddy weeder machine.


Palizi linafanyika siku kumi baada ya kupanda, na litafanyka hadi mara nne kwa kipindi cha uhai wa mpunga.

Faida tatu za aina hii ya palizi

  1. 1.       Kwanza kifaa huki huzika majani katika udongo na kuwa mbolea (green manure)


  1. 2.       Udogo husumbuliwa na kufanya hewa iingie ardhini, inafaida kwa mizizi na viumbe hai waboreshaji wa ardhi.


  1. 3.       Kifaa hiki hukatakata mizizi ya mimea iliyo kandokando. Kitendo hiki huakikisha mizizi mipya inakua na yenye uwezo mkubwa wa kujitafutia chakula na madini ardhini.



UMWAGILIAJI

Unamwagilia, ardhi ikiisha lowana unafungulia maji. Unaliacha shamba hadi litakapo kauna na ardhi kuanza kupasuka, hapo unamwagilia tena  na kufungulia maji kicha unaacha likauke tena hadi ardhi ianze kupasuka tena. Mzunnguko huu unaweza kufanyika kila baada ya siku saba hadi mmea utakapoanza kuzaa.

FAIDA YA MFUMO HUU WA UMWAGILIAJI

1.       Wadudu na bakteria wenye manufaa wanapata fursa ya kurutubisha udogo na kufanya rdhi iwe yenye kufaa Zaidi.
2.       Unasidia kuokoa maji amabyo yanaweza kutumika katika matumizi mengine ya shamba.


Mwisho

Ubunifu na majaribio ya mbinu tofauti tofauti katika kilimo ni muhimu ili ujipatie mavuno mengi.
Njia hii inatumika sehemu nyingi duniani. Kwa tanzania kuna tafiti zinaendelea na majaribio yameshaanza kuleta tija kwa mamia ya wakulima.

kwa tanzania kuna mbuyuni and kilimani skimu za umwagiliaji, shamba darasa kijiji cha kisegese mkoani mbeya, moshi iringa na maeneo mbailimbali matokeo mazuri ya mbiu hii yameanza kuonekana. 


1 comment:

  1. Ni kilimo safi na bora kwa mkulima anayetaka mabadiliko ya kianalojia

    ReplyDelete